Akiongea juu ya tukio hilo Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu TTCL nchi Dk Kamugisha Kazaura alisema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la soko la sovya majura ya saa kumi na moja alfajiri. Alisema kuwa wananchi wanaoishi karibu na eneo lililokatwa nyaya hizo ndiyo waliowakamata vijana hao baada ya kufanya uhslifu huo. Mkurugenzi huyo alisema kuwa hasara waliyoipatia kampuni kwa kukata nyaya hizo inakadiliwa ni zaidi ya milioni 20.
"Hasara waliyoingizia serekali ni kubwa sana hizo nyaya walizokata zinagharimu milioni 20,lakini kuitengeneza upya line hiyo inaweza kugharimu zaidi ya hiyo fedha''alisema Kazaura
Alisema kutokana na wezi huo umepelekea baadhi ya ofisi za serekali kukosa mawasiliano ikiwemo ofisi ya polisi Wilaya,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Bank na Takukuru. Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano profesa Makame Mbawala alivitaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya wezi hao wanaohujumu mawasiliano.
"Hawa muwapeleke kwenye sheria hiki walichofanya ni kosa kwa sheria ya mwaka 2015 wanatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni 50 au kifungo jela ili iwe fundisho kwa wengine" alisema profesa Mbawala
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment