Aneth David… Msichana Msomi wa Chuo Kikuu DSM Tanzania Aliyeshinda Tuzo ya Mwanasayansi Afrika

Tanzania imepata headlines nyingine baada ya kupata mshindi msomi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Aneth David ambaye pamoja na Waafrika wengine, wameshinda tuzo ya Mwanasayansi mkubwa ajaye duniani

Tuzo inaitwa Next Einstein Forum Ambassador na imeandaliwa na taasisi ya Next Einstein Forum ambao wanaamini kwamba Einstein anaekuja ambaye alikua Mwanasayansi mkubwa wa Marekani atatoka Afrika, Mwanasayansi huyu aliweza kutabiri mambo yaliyokuja kutokea miaka 100 baadae.

‘Next Einstein Forum wanaamini kuna Wanasayansi wanaofanya mambo makubwa na mazuri na yanasaidia jamii zao lakini wamefichika wapo vichakani, kinachojulikana zaidi kutoka Afrika ni vita njaa na magonjwa’ – Aneth

Aneth amesema alipeleka maombi ya kushiriki tuzo hii July 2015 na baadae akapata majibu, kulikua na Watanzania kama watano aliowaona walioshiriki kama yeye lakini yeye ndio akatajwa mshindi, kulikua na Wawakilishi 54 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo kila nchi imepata mwakilishi wake, yeye kashinda kuiwakilisha Tanzania.

March 2016 washindi walikutana Senegal kwenye mkutano mmoja na Mawaziri wa Sayansi Afrika na Marais akiwemo Rais Paul Kagame wa Rwanda na kuwaleta pamoja na Wadau wa sekta binafsi, hii ni kama kuileta dunia pamoja na Washindi hawa wanapata nafasi ya kuonyesha project zao za kuleta mabadiliko kwenye kizazi hiki.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment