Viatu
vya kimasai na zana nyingine zinazotumika kama urembo ambavyo
vimetajwa kama zana muhimu zinazotumiwa katika usafirishwaji wa madawa
hayo.
Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI
DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Tanzania kwenye viwanja
vya ndege vilivyopo nchini limekuwa likipambana na wauza madawa ya
kulevya ‘unga’ kwa kugundua na kuzima mbinu zote wanazotumia kusafirisha
biashara hiyo haramu, hivyo kupunguza kasi ya uingizwaji na utoaji wa
unga kwa njia ya ndege, UWAZI limeambiwa. Akizungumza na gazeti hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika wiki iliyopita Makao Makuu ya Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania yaliyopo jijini Dar, Kamanda wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno (pichani) alizitaja mbinu kumi wanazotumia wauza unga hao kusafirishia bidhaa hiyo.
“Kwanza napenda kuweka wazi kuwa, kwa sasa hatuna mchezo na wauza unga. Mbinu zao zote wanazotumia kusafirishia madawa yao tunazijua. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambia wauza unga wote kwamba, hakuna atakayepona safari hii,” alisema Otieno.
Kiatu cha kimasai kikiwa kimesheheni mzigo.
Akaendelea: “Wamekuwa wakisafirisha unga kwa kuhifadhi ndani ya
magogo. Gogo linapasuliwa wanaweka unga humo. Barabarani askari wanajua
ni magogo tu. Wengine wanatumia vinyago. Wangine wanaingiza unga kwenye
vipuli vya magari.Kamanda Otieno akaendelea: “Lakini pia mbinu nyingine kubwa ni kuweka kwenye sendozi za Kimasai. Wanaweka unga katikati ya soli na sehemu ya kukanyagia, kisha wanashona. Wanapokaguliwa, wanasema ni sendozi wanapeleka kuuza mikoani, kumbe katikati kuna unga. Pia wanatumia hereni nene, kwenye soksi na bangili nene.
“Sasa hivi kuna mbinu nyingine, wanachukua vitunguu, wanakata na kuondoa nyama za katikati, wanaweka vipaketi vya unga, wanafunika. We ukiangalia hivi unaona vitunguu.
Moja ya kipuli cha gari kikiwa kimeshindiliwa mzigo wa madawa hayo haramu.
“Pia wapo wanaotumia sabuni za vipande, wanachimba katikati na kuweka
unga humo, wanavirudishia na kuviweka kwenye maboksi kama bidhaa
inayopelekwa kuuzwa kwa matumizi ya kufulia. Pia wengine wanatumia pindo
za suruali, wanaingiza unga katikati. Mbinu hizo na nyingine kibao
tunazijua, wasirogwe.“Vigogo hao wamekuwa wakijifanya wanasafirisha vitu hivyo wanavyofichia madawa ya kulevya kama biashara lakini kutokana na ujuzi tulionazo pamoja na vifaa na mbwa tumekuwa tukiwakamata. Nina uhakika kuwa biashara hii inazidi kutoweka na ipo siku itakwisha kabisa.”
Kamanda Otineo aliendelea kusema kuwa, ni kazi ngumu kupambana na wauza unga kwani wamekuwa wakibuni mbinu kila kukicha lakini polisi na vyombo vingine vya dola wamejipanga vizuri kuhakikisha hakuna anayepitisha biashara hiyo katika viwanja vya ndege nchini.
Alisema mafanikio mengine yanatokana na ushirikiano wa wananchi hivyo amewaomba kuendelea kushirikiana kwani vita dhidi ya madawa ya kulevya siyo ya serikali peke yake.
-GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment