Tingatinga likiweka kifusi ndani ya gari kwenye Barabara ya Kijitonyama, Sinza, Dar.
Gari maalumu kwa ajili ya kushindilia udongo likiwa eneo la barabara hiyo.
Taswira ya eneo la barabara inayopita katika Zahanati ya Kijitonyama, Dar.
Kamera yetu imenasa ujenzi unavyoendelea katika eneo la Barabara ya Kijitonyama, Dar inayopita katika Zahanati ya Kijitonyama.
Mwandishi wetu alikuta ujenzi wa barabara hiyo ukipamba moto, huku magari ya kuondoa kifusi yakiingia na kutoka baada ya kujaza kifusi kilichokuwa kikiondolewa barabarani hapo kwa ajili ya maandalizi ya kuwekwa lami ambapo alizungumza na mkandarasi anayesimamia ujenzi huo Eng. Godson Tenga ambaye alisema:
“Ujenzi huu husimamiwa na kampuni yetu ambayo imekuwa ikijishughulisha na masuala ya ujenzi wa barabara hapa mjini na tenda nyingine mbalimbali.”
Alisema kuwa mradi huo una urefu wa kilomita 2.4 na upo chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni lakini alidai kuwa kuna changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo suala la miundombinu ya mabomba ya maji yanayowalazimu kungojea ili kuhamishiwa sehemu nyingine.
Na Denis Mtima/Gpl
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment