WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA
YAH: TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSU WALIMU KUSHONEWA SARE INAYOSAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi inakanusha taarifa
inayosambazwa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari
“NDALICHAKO NA WALIMU TZ”.
Taarifa
hiyo inadai kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof.
Joyce Ndalichako amesema kuwa walimu wanaandaliwa sare watakazo vaa
wakati wa kazi.
Tunapenda
kuufahamisha umma kuwa Taarifa hizi si za kweli. Aidha, Wizara
inawataka watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya
hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza.
Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
07/04/2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment