Kama bado unajiuliza nini kitatokea ndani ya klabu ya Man United
mwishoni mwa msimu, jibu bado litakuwa gumu kupata kwa kuhisi tu, April
11 2016 mitandao ya soka barani Ulaya imeandika stori mbili kubwa
ambazo ni ngumu kupata jibu kama Louis van Gaal atatimuliwa Man United mwisho wa msimu na Jose Mourinho kuchukua nafasi yake au la.
Baada ya Jose Mourinho kuripotiwa kuipotezea ofa ya kuifundisha timu ya taifa ya Syria, uamuzi huo ulizidisha tetesi kuwa Mourinho huenda akajiunga na Man United kweli, kinachoshangaza ni kuwa alikuwa anahusishwa kujiunga na Man United mwisho wa msimu, lakini Louis van Gaal anaripotiwa kuanza mipango ya usajili mwisho wa msimu.
Louis van Gaal ambaye ndio kocha wa sasa wa Man United anaripotiwa kuanza mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic, ripoti hiyo inafanya mashabiki wa soka kuanza kuhisi kuwa huenda mwisho wa msimu Man United wakafanya maamuzi yasio tarajiwa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment