Akizungumza na mtembezi.com wakati akitolea ufafanuzi kuhusu viongozi watatu wa upinzani kupewa nafasi katika baraza la uwakilishi, Dk. Jesse amesema nafasi aliyoipata Hamad Rashid itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha chama chake cha ADC na kukididimiza Chama cha Wananchi (CUF).
Amesema hakuna kifungu cha sheria katika Katiba ya Zanzibar kinachomzuia Rais kumteuwa mtu yeyote hivyo anampongeza Dk. Shein kwa kuwateuwa wapinzani katika nafasi za uwaziri na ujumbe wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa serikali itaimarika kwa kushirikiana na viongozi wenye sifa hata kama wanatoka upinzani.
Hivi karibuni Dk. Shein alifanya uteuzi wa Baraza la Mawaziri na kumteuwa Hamad Rashid kuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi huku Juma Ali Khatibu pamoja na Said Soud Said kuwa Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment