JAPAN YAJITOSA KUIKOPESHA TANZANIA BILIONI 116

Hivi karibuni Tanzania iliingia katika vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimeipelekea kukosa shilingi Trilioni moja kutoka bodi ya wakurugenzi wa shirika la changamoto za Milenia (MCC) kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar.

Lakini shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Wizara ya Fedha na Mipango wameweka saini mkataba wa mkopo kutoka Japan kwa ajili ya mradi wa maendeleo uitwao “Bussiness Environment for Jobs Development Policy Operation”wenye thamani ya fedha za kijapan (Japanese Yen) bilioni 6 sawa na shilingi bilioni 116 za kitanzania.

Akizungumza kuhusu mradi huo muwakilishi mkuu wa JICA Tanzania Toshio Magase amesema mradi huo unahusisha mfululizo wa mageuzi ya sera za maendeleo ambao utaweza kuondoa vikwazo katika mazingira muhimu ya bishara nchini Tanzania hasa katika viwanda na sekta zinazotoa ajira.

Magase ameongeza kuwa mradi huo utashughuikia maeneo makuu yenye vikwazo kwa kurahisisha, usajili, wa biashara na upatikanaji wa leseni ili kuimarisha ufanisi na umahiri wa utawala wa forodha, hasa katika bandari ya Dar es Salaam, ili kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment