Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau.
“Hili jambo halikubaliki na kama tuhuma
hizi ni za kweli, basi tunamuomba Rais John Magufuli amchukulie hatua za
kisheria kama wanavyofanyiwa wakubwa wengine waliolitia taifa letu
hasara. Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeweza kutumiwa
kutatua kero mbalimbali zinazotukabili Watanzania,” alisema msomaji
aliyejitambulisha kwa jina la Seve Nyari kutoka Singida.
Joji Salum, aliyepiga simu kutoka
Kigamboni, Dar alisema ni kweli mradi wa ujenzi wa Jiji Jipya la
Kigamboni umesimama na hawajui ni kwa sababu gani, lakini kwa ufisadi wa
fedha zinazotajwa, hakuna jinsi zaidi ya kumsulubu Dau ambaye
aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa balozi lakini bado hajapangiwa kituo
cha kazi kwa sababu alishiriki kwa asilimia mia moja si kwa kuzichukua
bali kama mtendaji mkuu.
Kutoka Arusha, ambako NSSF inaendelea na mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba wilayani Arumeru, Maige Joseph alisema:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
“Wakati umefika kwa mifuko ya jamii kama
huu, kudhibitiwa katika uanzishaji wa miradi yake, kwani mingi ni ya
kifisadi yenye kuwanufaisha wakubwa.
“Sasa mtu una ardhi yako, lakini
unanunua tena ya mtu mwingine, tena kwa bei ghali zaidi. Yaani unatoka
kilometa 30 kutoka Arusha mjini, unakwenda kununua heka moja kwa
shilingi bilioni moja!? Hii haijapata kutokea, labda Tanzania tu.
Wasulubiwe walioshiriki,” alisema Maige.
Akaongeza: “Nasema Dau anahusika kwa
sababu si ndiyo alikuwa bosi mkuu? Maana yake ni kwamba hakuna
kilichokuwa kikifanyika bila ya yeye kujua. Ni lazima anajua mwanzo
mwisho. Mimi naona hata huo ubalozi ungetenguliwa tu kwani ameacha doa
NSSF.”
Kauli ya kutaka watu wote waliohusika kufisadi fedha hizo wasubulubiwe,
pia ilitoka kwa wananchi waliopiga simu kutoka Mwanjelwa Mbeya, Tukuyu
(pia Mbeya), Iringa mjini, Mtwara, Simiyu, Kondoa (Dodoma), Tanga na
Mwanza.
Ufisadi ulioibuliwa hivi karibuni ni
kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kinadaiwa kutumiwa na NSSF katika
mazingira yanayotia shaka katika ununuzi wa ardhi ili kutekeleza miradi
miwili ya ujenzi wa nyumba huko Kigamboni na Arumeru mkoani Arusha.
Jijini Dar es Salaam, mfuko huo ulianzisha mradi uitwao Dege Eco Village
ambao Bodi ya NSSF iliunda Kampuni ya Hifadhi Builders inayosimamia
ujenzi huo ikishirikiana na Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited.
Inadaiwa Azimio Housing Estate
inayomiliki ekari 20,000 huko Kigamboni, iliiuzia NSSF eneo la ekari 300
kwa shilingi milioni 800 kwa ekari moja, badala ya bei halali ya
shilingi milioni 39 kwa ekari tofauti na bei iliyotangazwa na Manispaa
ya Temeke mwaka 2012 wakati ikiuza eneo lake kwa shilingi elfu nane kwa
mita ya mraba.
Katika ujenzi wa Arumeru, inadaiwa
kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni
1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo
lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya
shilingi laki tano hadi milioni moja.
Uchunguzi unaonesha Azimio iliuza eka
300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113 (sawa na madafu bilioni 217.8),
wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa ekari 655 kwa dola 556, 764, 924
(trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla ya fedha ambazo ‘zimeliwa’
katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke yake kufikia trilioni 1.3.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment