UAMUZI
wa ombi la kufutiwa mashitaka ya utakatishaji wa fedha lililowasilishwa
na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry
Kitilya na wenzake, unatarajiwa kutolewa Aprili 27 mwaka huu.
Uamuzi
huo ulitakiwa kutolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
lakini Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Emillius Mchauru, aliahirisha
kwa sababu hajamaliza kuuandika.
Hakimu
Mchauru alisema, alipewa majukumu mengine ya kikazi, akashindwa
kuandika uamuzi huo, lakini imebaki sehemu ndogo hivyo atausoma Jumatano
ya Aprili 27, mwaka huu.
Mbali
na Kitilya, wengine katika kesi hiyo ni mrembo wa zamani wa Tanzania
ambaye pia alikuwa Mkuu wa Uwekezaji wa Benki ya Stanbic, Shose Sinare
na aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa benki hiyo, Sioi Graham
Solomon.
Washitakiwa wote wapo rumande kwa kuwa kisheria mashitaka ya utakatishaji wa fedha ambayo wanaomba yafutwe hayana dhamana.
Katika
ombi lao walilowasilisha kupitia jopo la mawakili likiongozwa na Wakili
Alex Mgongolwa, waliiomba Mahakama iwafutie mashitaka hayo kwa kuwa
hati ya mashitaka haina maelezo yanayokidhi vigezo vya kisheria vya
mashitaka hayo.
Mgongolwa
alidai ili mashitaka yawe ya utakatishaji wa fedha, ni lazima kuwe na
hatua nne; kwanza kuwe na kuwekwa kwa fedha, kuhamishwa kwa fedha na
fedha kuwekwa kwenye shughuli za kiuchumi kwa lengo la kuficha, pia kuwe
na chanzo kichafu cha fedha.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment