Mchezaji wa Simba Hamis Kiiza Afunguka Baada ya Kutimuliwa Kambini... Adai Anachafuliwa Jina

Kocha wa Klabu ya Simba, Jackson Mayanja amemfukuza kambini mshambuliaji Hamis Kiiza kufuatia tuhuma ya Utovu wa Nidhamu kambini.
Alipotafutwa Kiiza kuzungumzia sakata hilo, akasema anaona kama anatafutiwa sababu ya kuchafuliwa jina. “Mimi naona kama wanataka kunigombanisha na timu. Jana asubuhi tumemaliza mazoezi (Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini), tukaambiwa jioni tutaingia kambini, lakini kwanza tutakula chakula cha mchana pamoja na kwenda Uwanja wa Taifa,”. Kiiza anasema kwamba Meneja wa timu, Abbas akaagiza wachezaji wote wavae sare wakati wa kukutana kwa chakula cha mchana na wasije na gari zao, kwa sababu watapanda basi la timu.

Hata hivyo, Kiiza anasema kwamba alimfuata kocha Mayanja na kumuambia kwamba ameitwa kwenye kikao na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Kassim Dewji hivyo anahisi atachelewa chakula cha mchana cha pamoja. “Mayanja akaniambia hayo mimi hayanihusu, mwambie Meneja. Mimi nikamuambia Meneja, akanielewa nikaondoka zangu,”anasema Kiiza.

Anasema alikwenda kukutana na Dewji katika kikao kilichodumu hadi Saa 9:15 Alasiri ndipo wakaachana na kwa sababu muda ulikuwa umekwenda sana, akaamua kwenda Uwanja wa Taifa moja kwa moja ili akitoka ndiyo arejee nyumbani kwake kuchukua sare na vifaa vya kambini. “Baada ya mechi Abbas akanipigia kuniambia Kiiza usije kambini kwa sababu umekataa kupanda basi la timu na kuvaa sare. Mimi nikashangaa sana, kwanza muda mwingi tunapokuja mazoezini tukitokea nyumbani huwa hatubebi sare. Na hata Juuko (Murshid) na (Jonas) Mkude hawakuja na basi la timu pia,” “Lakini mimi nikamuambia Abbas kama unataka nisiingie kambini, mwambie bosi (Dewji) aniambie hivyo kwa sababu yeye ndiye shahidi yangu nilikuwa naye kwenye kikao.


Abbas akasema sitaki kujua hayo. Mimi nikampigia Dewji kumuambia, yeye (Dewji) akawapigia akina Abbas. Akanirudia mimi akaniambia niende kambini na yeye anakuja. “Nilipofika kambini, Mayanja akanikuta akaniuliza, Abbas amekupa ujumbe wako? Nikamuambia amenipa, lakini Dewji amezungumza naye nadhani ameelewa, ikawa kama yamekwisha,” amesema Kiiza.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment