Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bweya katika Kijiji cha Bweya mkoani Geita,
Augustine Katemi (42) ameuawa baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na
mke wa mtu vichakani.
Mwenyekiti huyo alifariki dunia papohapo
baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa sime na mume wa mwanamke huyo, mkazi
wa Kijiji cha Luchili, Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.
Tukio hilo lilitokea saa nne usiku Machi 28 baada ya marehemu kudaiwa kukutwa akifanya tendo la ndoa na Chausiku Isangula (32).
Hata
hivyo, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,
Latson Mpojoli alisema hana za taarifa za tukio hilo na kuahidi kufuatilia.
Ilielezwa
kuwa Katemi aliuawa baada ya kushambuliwa kwa sime na kufa papohapo na
baada ya tukio hilo, mtuhumiwa anadaiwa kumshambulia mkewe kwa kutumia
sime hiyohiyo na kumsababishia majeraha makubwa sehemu mbalimbali za
mwili na amelazwa kwenye Kituo cha Afya cha Nzera.
Mtendaji wa
Serikali ya Kijiji cha Bweya, Samson Walwa alisema baada ya kutokea
tukio hilo wananchi waliendesha msako na kumtia mbaroni mtuhumiwa wakati
akijaribu kutoroka kuelekea Sengerema.
Walwa alisema mtuhumiwa
alikamatwa nyumbani kwa Edward Iswalala alipokuwa amefikia kwa siri
kutoka Luchili ili kufuatilia mwenendo wa mkewe ambaye anadaiwa kuwa
awali alimuaga kuwa anakwenda kumsalimia baba yake mzazi anayetibiwa kwa
mganga wa kienyeji.
“Inavyosemekana alikuwa akifuatilia
mienendo ya mke wake… sisi tulipomkamata tumemkabidhi Kituo cha Polisi
cha Nzera pamoja na nguo za marehemu (mwenyekiti) na zile za mkewe kwani
alipofanya mauaji hayo alizichukua nguzo zao hadi tulipomkata nazo,” alisema Walwa.
Mmoja
wa wananchi walioshuhudia tukio hilo, Jumanne Tole alisema, Chausiku
alimuaga mumewe kuwa alikuwa anakwenda kijiji cha Kalebezo kumsalimia
baba yake mzazi kwa waganga wa tiba asilia alikokuwa anatibiwa lakini
baada ya kufika na kumsalimia, alikwenda kwa kaka yake aitwaye
Ndagabwene Isangula huko Bweya alikofikwa na mkasa huo.
Alisema
kuna madai kuwa mtuhumiwa alifika kijijini hapo kwa siri akiwa amevaa
nguo na kofia zilizochakaa ili asifahamike wakati akifuatilia nyendo za
marehemu na mkewe na akafanikiwa ikidaiwa kwamba alikuwa na watu ambao
walikuwa wakimpatia taarifa hizo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment