Ofisi ya Waziri Mkuu itatumia usafiri wa bajaji na bodaboda kuendesha
shughuli zake kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/2017 ikiwa ni mkakati
wa kubana matumizi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Mpango huo umo
kwenye hotuba ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyosomwa
jana bungeni na Kassim Majaliwa, na baadaye kusifiwa na mwenyekiti wa
Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge, Mohamed Mchengerwa wakati akisoma
maoni ya kamati kuhusu bajeti hiyo.
Wizara iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu.
Akiwasilisha
maoni ya kamati hiyo, Mchengerwa alisema uamuzi wa aina hiyo unaendana
na dhana ya kubana matumizi ya fedha wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Hata
hivyo, hotuba iliyosomwa na Waziri Majaliwa haijaeleza pikipiki hizo za
magurumu mawili na matatu zitatumiwa na watumishi wa kada gani.
Serikali
ya Awamu ya Tano imekuwa kwenye mkakati mkali wa kubana matumizi
yasiyo ya lazima na tayari Rais John Magufuli ametangaza kuwa kuanzia
mwaka mpya wa fedha hakuna mtumishi wa umma atakayelipwa zaidi ya Sh15
milioni, huku akifuta sherehe za maadhimisho ya siku za kitaifa,
zikiwamo za Muungano na Uhuru.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
Katika
maoni yake, kamati hiyo imeitaka Serikali kutoa tamko kuhusu maandalizi
na utekelezaji wa mchakato wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Pia
kamati hiyo ilitaka Nec kuweka utaratibu mpya wa ratiba ya upigaji kura
ili chaguzi zote za rais, wabunge, madiwani na viongozi wa Serikali za
mitaa zifanyike kwa wakati mmoja.
“Hii itasaidia kupunguza
gharama zinazotumika kwa nyakati mbili tofauti pamoja na kusaidia
kupunguza mtikisiko wa amani nchini,”alisema.
Uchaguzi wa
viongozi wa Serikali za mitaa hutangulia takriban mwaka mmoja kabla ya
Uchaguzi Mkuu ambao huhusisha uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment