Samia amewasili mjini Morogoro majira ya asubuhi hii jana na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo na baadaye kupokea taarifa ya mkoa katika ikulu ndogo ya mkoa.
Makamu huyo wa Rais yuko mkoani Morogoro kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru utakaowashwa kitaifa mkoani humo ambapo amesema lengo la kuwawajibisha watumishi wasio waadilifu ni kutaka kuondoa “gepu” kubwa lililopo kati ya walionacho na wasiokuwanacho ili kudumisha amani na utulivu miongoni mwa watanzania.
Akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za mwenge Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephene Kebwe amesema maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa licha ya kuwepo changamoto ndogondogo za miundombinu ya barabara kukatika ambapo amesema wahandisi na wakandarasi wanafanya jitihada za haraka kurejesha mawasiliano ya barabara hizo.
Mwenge wa uhuru utawashwa April 18 mwaka huu katika uwanja wa shule ya msingi Mwembesongo Mkoani Morogoro na baadaye kukimbizwa katika wilaya zote za mkoa huo kabla ya kukabidhiwa katika mkoa wa Iringa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment