SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA.
Katika Mkutano huu shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kiapo cha uaminifu kwa wabunge wapya wanne ambao ni Mhe Shamsi Vuai Nahodah (Jimbo la Kijitoupele), Mhe. Ritha Kabati (Viti Maalum), Mhe. Lucy Owenya (Viti Maalum) na Mhe. Oliver Semguruka (Viti Maalum)
Aidha, katika mkutano huu pia Bunge litanatarajia kujadili na kupitisha Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano 2015/16 – 2020/21 kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili 2016.
Baada ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano kukamilika Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa bajeti kwa Wizara zote kwa mwaka wa Fedha 2015/16 pamoja na makadirio ya matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17 kazi itakayofanyika kuanzia tarehe 22 Aprili hadi 2 Juni 2016.
Siku ya Alhamisi tarehe 9/Juni/2016 saa 4:00 Asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 itakayosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango Saa 10:00 jioni.
Mjadala kuhusu Bajeti ya Serikali utafanyika kuanzia tarehe 13/06/2016 hadi tarehe 21/06/2016.
HATI ZA KUWASILISHA MEZANI
Katika Mkutano huu pia kutakuwa na Hati za Kuwasilisha Mezani ambapo Bunge lipatokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2014/15 pamoja na majibu ya Serikali kuhusu hoja zilizotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za mwaka wa Fedha 2014/15.
Pamoja na shughuli hizo, jumla ya maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali Bungeni katika Mkutano huu ambapo kila alhamisi yataulizwa Maswali kwa Waziri Mkuu na jumla ya maswali 88 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na Mhe. Waziri Mkuu.
MISWADA YA SERIKALI
Katika Mkutano huu, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha Miswada Miwili ambayo ni Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2016 pamoja na kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2016.
Vilevile inategemewa kwamba Serikali itawasilisha Bungeni Miswada ya Sheria kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa Bungeni mara baada ya shughuli za kupitisha Bajeti kukamilika. Kuwatakuwa pia na uchaguzi wa Mwenyekiti mmoja wa Bunge ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi baada ya Mhe Spika kufanya mabadiliko ya Wajumbe wa baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge.
HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE
Shughuli za Mkutano wa Tatu zinatarajiwa kumalizika tarehe 01 Julai, 2016 kwa Hoja ya kuahirisha Bunge itakayotolewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment