Mayanja amesema kasi ya wachezaji katika kuipa heshima klabu lazima ibadilike na hilo litaanzia kwa kutwaa ubingwa, ambapo leo wanacheza raundi ya 25 kwa kuvaana na Toto Africans Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba ni moja ya timu tatu zinazopigania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu, hasa baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la FA Jumatatu iliyopita kwa kufungwa mabao 2-1 na Coastal Union ya Tanga katika Nusu Fainali.
Mayanja alisema huu ni wakati muhimu kwa wachezaji wake kucheza kwa juhudi na kuhakikisha Simba inabeba ubingwa ili wajitengenezee mazingira ya kubaki msimu ujao wa ligi.
“Hiki ndiyo kipindi pekee ambacho wachezaji wanapaswa kutengeneza soko lao la usajili kwa kuipigania Simba kubeba ubingwa, kwa sababu tukikosa na taji hili hata kazi waliyofanya huko nyuma haitaonekana na watatafutwa wachezaji wapya,” alisema Mayanja.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment