SIKU
moja baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kususa kuchangia hotuba
za bajeti, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri,
amesema serikali haikukosea kuipa Wizara ya Ujenzi fedha zaidi ya
zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge.
Hoja hiyo ni moja kati ya tatu ambazo juzi ziliibuliwa bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Badala
ya kuwasilisha Mpango Mbadala wa Maendeleo wa Taifa na maoni ya Kambi
Rasmi ya Upinzani kuhusu mpango wa serikali pamoja na maoni ya kambi
hiyo kuhusu hotuba ya Waziri Mkuu, juzi Mbowe alisema wabunge wa
upinzani watakuwa wanaingia kwenye Ukumbi wa Bunge lakini hawatachangia
hotuba ya bajeti mpaka pale hoja zao zitakapojibiwa.
Mbowe
alidai kuwa uamuzi wao huo umetokana na Serikali kufanya kazi bila kuwa
na mwongozo wa utendaji kazi kwa wizara mbalimbali, kuvunjwa kwa Katiba
na sheria za nchi na kupokwa uhuru na madaraka ya muhimili wa Bunge.
Mwenyekiti
huyo wa Chadema na Mbunge wa Hai, alikwenda mbali zaidi akieleza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imekiuka sheria kwa kuipatia Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Sh. bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani kwa
ajili ya bajeti ya maendeleo ya mwaka wa fedha 2015/16 wakati Bunge
liliidhinisha Sh. bilioni 191.6.
Wakati
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyeongoza kikao cha juzi akieleza
kuwa madai ya upinzani ni mazito na kushauri waende mahakamani,
Serikali imejibu moja ya hoja tatu za Mbowe.
Akiongea
na waandishi wa habari katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango
jana asubuhi, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Mwanri, alisema
Serikali ya Awamu ya Tano haijafanya makosa kuipa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano kiasi hicho cha fedha.
Ofisa
huyo wa serikali alisema Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa
Masuhuli na Waziri kufanya uhamisho wa fedha za mradi mmoja kwenda
kutekeleza mradi mwingine.
"Sheria
ya Bajeti ya Mwaka 2015 inaruhusu Ofisa Masuhuli kufanya 'reallocation'
(uhamisho) ya matumizi ya fedha lakini isizidi asilimia saba ya 'Vote'
(Fungu) husika," alisema na kuongeza:
"Sheria
hiyo pia inamruhusu Waziri kufanya 'reallocation' ya matumizi ya bajeti
husika lakini haipaswi kuzidi asilimia 10. Pesa ilizopewa Wizara ya
Ujenzi zimezingatia sheria na fungu walilopewa limo ndani ya sheria."
Florence
alisema wizara hiyo ina madeni makubwa ya wakandarasi, hivyo kutoyalipa
ni kuendelea kukuza mzigo kwa serikali kwa kuwa riba inaongezeka.
"Serikali
iliamua kutoa kiasi hicho cha fedha (Sh. bilioni 607.4) ili kuyapunguza
madeni ya Wizara ya Ujenzi. Tukumbuke kuwa wizara hii, ndiyo yenye
madeni makubwa," alifafanua zaidi ofisa huyo wa serikali.
Katika
maelezo yake ya msingi aliyoyawasilisha bungeni juzi, Mbowe alisema
kuwa kwa kuipa wizara hiyo kiasi hicho cha fedha badala ya Sh. bilioni
191.6 zilizoidhinshwa na Bunge, Serikali ya Awamu ya Tano imevunja
kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015.
Kwa
mujibu wa Katiba hiyo, kifungu hicho kinasema: “Serikali itawasilisha
bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo
zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya
kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.
Mbowe
alisema utaratibu huo pia unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa
mwaka 2001 (Public Finacne Act, 2001) ambayo kifungu cha 18 (3) na (4)
inaitaka serikali kupeleka bungeni bajeti ya nyongeza (mini-budget) kwa
ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali
hazikutosha
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment