Umoja
wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu Frederick
Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa
kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala
ya utawala.
Sumaye
ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli
ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu
lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa.
Msimamo
huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka
alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na
mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro.
Shaka
alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu
kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka
nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani
wananchi wameyasahau.
Alisema
kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na
usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita
Sumaye.
Aidha
Kaimu huyo alimuonya Sumaye kuacha kumfuatafuata Dk Magufuli katika
mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazozichukua dhidi ya
mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema
wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi
kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima kina sumaye na
wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa
ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
Pia
shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Rombo kujitayarisha ili kumpiga
chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwa
sabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
"Siku
zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, Selasimi hajui
anachokifanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo
lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka
Akizungumza
katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib
Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya
kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali kwa
ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu
alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya
Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi
ya asili au ujamaa.
"Tunachotaka
kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa
Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, hakutuacha tukiwa tumegawanyika ,
tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni
kwasabahu hilo ni balaa au janga katika jamii "alisema Raib.
Jumla
ya wanachama wapya 103 walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka
alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za
makiidi na mahare wilaya ya Rombo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment