ZITTO KABWE ATUA MAREKANI, KUHUTUBIA WABUNGE WA DUNIA NA KUSOMA KOZI CHUO CHA HARVAD

KIONGOZI wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto, anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wabunge kutoka nchi tofauti duniani ulioandaliwa na Benki ya Dunia nchini Marekani.
Kwenye mkutano huo, Zitto atatoa mada kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii kwa watu walio kwenye sekta isiyo rasmi. Pia atahudhuria kozi maalumu ya uongozi katika Chuo Kikuu cha Harvard, nchini Marekani.Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba, ilieleza kuwa Zitto atakuwa nje ya nchi kuanzia jana, Aprili 7 hadi Aprili 29 mwaka huu kwa shughuli mbalimbali ikiwamo kuhudhuria mkutano huo.

“Kutokana na safari hiyo na kwa mujibu wa Katiba ya ACT-Wazalendo ya mwaka 2015, Ibara ya 29 ibara ndogo ya (25) kipengele cha (xi), Kiongozi wa Chama amemteua Yeremia Kulwa Maganja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa Taifa, kukaimu nafasi ya Kiongozi wa chama kwa muda ambao hatakuwepo nchini,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mwigamba alisema, katika taarifa hiyo kuwa, uongozi na Mwenyekiti wa chama hicho wanamtakia Maganja utekelezaji bora wa majukumu yake kwa kipindi hicho.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment