Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John
Magufuli kukabiliana na vikundi vya mafisadi vinavyoiba mabilioni ya
fedha za umma kupitia mikataba mibovu waliyoingia badala ya kuishia
kutumbua majipu.
Akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya chama chake jana, Zitto alisema ACT Wazalendo inaunga mkono
jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, lakini bado
hajagusa kiini chenyewe.
Zitto alitolea mfano wa kashfa ya Akaunti
ya Tegeta Escrow kuwa bado kuna kampuni inayolipwa Sh8 bilioni kila
mwezi kwa ajili ya mitambo yake ya umeme.
Pia, alisema kashfa ya hati fungani imeongeza deni la Taifa kwa Sh1.2 trilioni.
“Bado
huo mtambo upo chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa Sh8
bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. Hivi ndivyo vikundi masilahi
katika sekta ya nishati. Bila kuvibomoa, Rais ataonekana anachagua watu
katika vita hii,” alisema Zitto.
Alisema: “Ni kweli kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya Dola 6 milioni za Marekani zinazohusu hati fungani.
"Serikali
imewafikisha mahakamani madalali wa rushwa lakini waliotoa rushwa hiyo
hawapo mahakamani. Waliopokea rushwa ambao ni maofisa wa Wizara ya Fedha
hawajashtakiwa.”
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema vita ya ufisadi siyo ya kutumbua majipu tu, bali kujenga mfumo madhubuti wa kuzuia mianya ya rushwa.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema vita ya ufisadi siyo ya kutumbua majipu tu, bali kujenga mfumo madhubuti wa kuzuia mianya ya rushwa.
Alisema Rais Magufuli anapaswa kuwaongoza Watanzania katika vita ya kukataa mikopo kama hiyo ambayo inawasababishia umaskini.
Aungana
na hoja za upinzani
Zitto alisema chama chake kinaungana na vyama
vingine vya upinzani kwa hoja walizozitoa baada ya kutoka bungeni za
kutokuonyeshwa moja kwa moja kwa matangazo ya televisheni kutoka
bungeni, matumizi ya Serikali nje ya mpango wa bajeti na Serikali
kutokuwa na mwongozo kwa mawaziri wake.
Akizungumzia kusitishwa kwa
urushaji wa matangazo ya Bunge, Zitto alisema hatua hiyo inatakiwa
kupigwa vita kwa sababu inajenga udikteta katika nchi na kuwanyima
wananchi haki ya kupata habari za Bunge.
“Ina maana TV zinapaswa
kumuonyesha mtu mmoja tu akihutubia bungeni ambaye ni Rais tu... hapana
hii siyo sawa,” alisema Zitto.
Akizungumzia suala la bajeti, Zitto alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka Rais kuhamisha fedha kwenda kufanya shughuli nyingine. Lakini alisema tangu Rais Magufuli achaguliwe, amekuwa akihamisha fedha wakati Bunge lilishapitisha bajeti.
Akizungumzia suala la bajeti, Zitto alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka Rais kuhamisha fedha kwenda kufanya shughuli nyingine. Lakini alisema tangu Rais Magufuli achaguliwe, amekuwa akihamisha fedha wakati Bunge lilishapitisha bajeti.
“Rais Magufuli kwani amekuwa waziri wa fedha,
waziri wa ujenzi na Rais kwa wakati mmoja? Tunamtaka asiingilie
majukumu ya mihimili mingine, wananchi tumnyooshee kidole na kumwambia
afuate utaratibu,” alisema Zitto.
Mbunge huyo pekee wa chama hicho,
alisema tangu walipoapishwa, mawaziri hawajapewa mwongozo wa kazi na
kutoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa miongozo kwa mawaziri.
“Mpaka sasa nchi haina mawaziri kwa sababu hawajapewa miongozo. Kwa
hiyo, Baraza la Mawaziri lina mawaziri wawili tu ambao ni Rais na
makamu wake,” alisema Zitto na kulitaka Bunge kutengeneza mfumo wa
kuisukuma Serikali kutekeleza mambo muhimu kwa Taifa.
Kuhusu hali ya
uchumi, Zitto alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka mpaka kufikia
Sh29 trilioni lakini ana wasiwasi itakwama kwa sababu theluthi moja ya
mapato ya ndani yanatoka bandarini ambako ripoti zinaonyesha kuwa
yamepungua.
Alisema Serikali imepanga kukopa Sh7 trilioni kwa ajili
ya utekelezaji wa bajeti na kwamba hatua hiyo inazidi kuongeza deni la
Taifa ambalo limelalamikiwa pia na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) katika ripoti yake.
Mwenyekiti wa ACT, Anna
Mghwira aliwataka wajumbe wa chama hicho kusimama pamoja ili kukijenga
chama hicho na kukifanya kiwe mbadala kwa Watanzania akisema kimewavutia
watu wengi ambao wanachukizwa na ufisadi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment