KAMATI
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
imepitisha majina ya wabunge 21 walioomba nafasi ya ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema Kamati Kuu ilifanya maamuzi hayo kupitia kikao chake kilichofanyika jana, Ikulu ya Chamwino Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa pia na Rais John Magufuli.
Pamoja
na kupitishwa kwa majina hayo, Kamati Kuu imewataka wagombea wote
kufuata sheria na taratibu za chama na kwamba atakayekiuka, atachukuliwa
hatua za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kuenguliwa kwa jina lake katika
nafasi za wagombea.
Waliopitishwa kuwania nafasi 10 za NEC kutoka Bunge la Tanzania kwa CCM ni
- Munde Tambwe,
- Jamal Kassim Ali,
- Faida Mohamed Bakari,
- Mbaraka Dau, Alex Gashaza,
- Hawa Ghasia,
- Ibrahim Hassanali Raza,
- Angela Kairuki,
- Dk Hamis Kingwangalla,
- Profesa Norman King,
- Livingstone Lusinde na
- Angelina Mabula.
Wengine
ni Almasi Maige, Angelina Malembeka, Agness Marwa, Yahaya Massare,
Steven Ngonyani ‘Maji Marefu,’ Stanslaus Nyongo, Mattar Ali Salum, Peter
Serukamba na Hafidh Ali Tahir.
Pia
Kamati Kuu imepitisha majina 19 ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,
walioomba kugombea nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia Baraza la Wawakilishi
Zanzibar.
Waliopitishwa
ni Nassoro Salim Ally, Ally Hamisi Bakari, Salma Mussa Bilal, Mgeni
Hassan Juma, Riziki Pemba Juma, Yussuph Hassan Idd, Khadija Omary
Kibano, Shamata Shaame Khamisi, Mmanga Mjawiri na Dk Khalid Salum
Mohamed.
Pia
wamo Aska Abdallah Mussa, Mihayo Juma N’hunga, Zulfa Mmaka Omar, Hamad
Abdallah Rashid, Mohamed Ahmada Salum, Harusi Saidi Suleiman, Haroun Ali
Suleiman, Issa Haji Ussi na Bahati Khamisi Kombo.
Aidha,
Sendeka alisema kuwa Kamati Kuu pia imepitisha majina ya wabunge wa CCM
wanne, walioomba nafasi ya Katibu wa Kamati ya Wabunge wote wa CCM.
Waliopitishwa
ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza, Mbunge wa Korogwe Mjini,
Mary Chatanda, Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kisangi na Mbunge wa
Mkuranga, Abdallah Ulega.
Nafasi
hiyo ilikuwa inashikiliwa na Mbunge wa Peramiho na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama.Katibu wa wabunge huingia moja kwa moja katika Kamati
Kuu.
Pia
imepitisha majina matatu ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walioomba
nafasi ya Katibu wa Kamati ya Wajumbe wa Baraza hilo kupitia CCM.Hao ni
Ali Suleiman Ali (Shihata), Ali Salum Haji na Abdallah Ali Kombo.
Msemaji
huyo wa CCM alieleza kuwa Kamati Kuu pia imepitisha majina ya wana CCM
walioomba nafasi wazi mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ambayo wamepitishwa Josephat
Ntambindi, Gilbert Kagoma na Malck Rudugu.
Kwa
nafasi ya Mjumbe wa NEC Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, waliopitishwa
ni Omar Kigoda, Maajabu Hamis, Mussa Kidato, Hamisi Mnondwa na Athuman
Lukoya.
Aidha,
nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha, Mkoa wa Mbeya, Sendeka aliwataja
waliopitishwa kugombea ni Charles Mwakipesile, James Mwasunga na Stephen
Mwakajumulo.
Kwa nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha, Mkoa wa Njombe waliopitishwa ni Creiton Lulambo, Salu Sanga na Erick Nyagawa.
Katika
hatua nyingine, Kamati Kuu imempongeza Dk Ali Mohamed Shein kwa
kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kwa kura nyingi katika uchaguzi wa
marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Aidha,
Kamati Kuu imewapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuendelea kukiamini
Chama Cha Mapinduzi kwa kukipa ushindi wa kishindo katika nafasi ya
Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani.
Wakati
huo huo, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka amesema chama hicho
kiko katika hatua za mwisho za makabidhiano ya nafasi ya Uenyekiti wa
Taifa kati ya Mwenyekiti wa sasa, Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.
Akizungumza
jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, Sendeka alisema
suala la kukabidhiana mikoba kati ya Kikwete na Rais Magufuli kwa mujibu
wa uzoefu wa CCM anayechaguliwa kuwa Rais kwa tiketi ya chama hicho
ndiye anayepokea nafasi ya uenyekiti wa CCM.
“Bahati
nzuri hawa wakubwa walikuwa wameshauriana kwamba Uenyekiti ni miaka
mitano, Dk Kikwete angeweza kuendelea kuwa mwenyekiti, lakini uzoefu wa
kupokezana vijiti na uongozi tangu wakati wa Rais mstaafu Ali Hassan
Mwinyi, Benjamin Mkapa na sasa ni Kikwete unaonesha kwamba umekuwa
ukifanyika mwaka unaofuata baada ya uchaguzi kwenye mwezi Juni,” alieleza Sendeka.
“Mwaka
huu wakubwa hawa walishashauriana,Kikwete alishatangaza wazi kwamba
anakusudia kumkabidhi nafasi ya uenyekiti Rais wa sasa, Dk Magufuli
wakati wowote mwaka huu na kinachofanyika sasa ni maandalizi .
"Tarehe
na mwezi ambao Mkutano Mkuu utafanyika tutawaarifu lakini tumekubaliana
tupo kwenye mchakato wa Mkutano Mkuu Maalumu ili Kikwete aweze
kukabidhi uenyekiti kwa Magufuli.”
Alisema
nafasi ya Mwenyekiti wa chama kikubwa kama CCM inapotokea mamlaka ya
Rais ipo kwa mtu mwingine inaweza kuleta mkanganyiko wa kudhoofisha
lengo la mtu aliyekabidhiwa nchi ya kuyafanya.
“Ni
mazoea na utamaduni wetu wa CCM kwamba Mwana CCM mwingine ataweza
kujitokeza kugombea hazuiwi Katiba ipo kanuni zipo ataelekezwa,” alisema Sendeka.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment