Mtoto
wa miaka mitatu aliyefahamika kwa jina la JANET PONSIAN mkazi wa
Matemela Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya alifariki dunia papo hapo baada
ya kugongwa na Gari yenye namba za usajili T.957 CWJ aina ya Isuzu
Journey ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ELIABU MYEKO
(33) mkazi wa Makambako Mkoa wa Njombe.
Tukio
hilo limetokea mnamo tarehe 01.05.2016 majira ya saa 17:45 jioni huko
katika Kijiji cha Matemela, Kata ya Ipwani, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya
Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa Dereva wa Gari hilo.
Dereva alikimbia mara baada ya tukio na jitihada za kumtafuta kwa
kushirikiana na mmiliki wa Gari zinaendelea. Mwili wa marehemu
umehifadhiwa Kituo cha Afya Ipwani Wilayani Mbarali kwa uchunguzi wa
kitabibu.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL G.
LUKULA anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto
ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa wito kwa
yeyote mwenye taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa dereva huyu
azitoe kwa mamlaka husika ili akamatwe.
Katika Misako:
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Matemela
aliyefahamika kwa jina la HUSSEIN BAKARI (59) baada ya kukutwa na miche
25 ya Bhangi akiwa amepanda kwenye bustani yake ya mbogamboga.
Mtuhumiwa
alikamatwa katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.02.2016 majira ya
saa 16:00 jioni katika Kijiji cha Mayota, Kata ya Lugelele, Tarafa ya
Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.
Aidha
katika msako mwingine, Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la WILSON
PHILIP (19) mwendesha Pikipiki @ bodaboda, mkazi wa Msasani anashikiliwa
na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya akiwa na Bhangi yenye uzito wa Gram
10.
Mtuhumiwa
alikamatwa na askari katika msako uliofanyika mnamo tarehe 01.05.2016
majira ya saa 17:05 jioni huko Mtaa wa msasani, Kata ya Bagamoyo, Tarafa
ya Tukuyu Mjini, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamiliki.
Imesainiwa na:
(EMANUEL G. LUKULA – ACP)
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment