Bi. Hillary Clinton Adai Hakufuata Ushauri Wa Madaktari Wake

Mgombea wa chama cha Democratic nchini Marekani Bi. Hillary Clinton amedai kuwa hakufuata vizuri ushauri wa madaktari wake ndiyo maana alizidiwa hadi kufikia hatua ya kuanguka kwenye sherehe ya kumbukumbu ya Septemba 11.

Bi. Clinton amesema kuwa madaktari wake walimtaka apumzike kwa muda usiopungua siku tano baada ya kufanyiwa vipimo hivyo siku ya Ijumaa. Aidha taarifa ya afya yake inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na viongozi wake wa kampeni.

Mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump anatumaini kuwa Bi. Clinton atapona siku siyo nyingi na kudai kuwa ugonjwa wa mgombea huo unaweza ukawa ni tatizo kwenye uchaguzi mkuu.

Bi. Clinton alianguka na kudakwa na walinzi wake na kuondolewa kwenye eneo la kumbukumbu ta majengo ya World Trade Center kwa gari maalumu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment