Daraja la vioo lililojengwa juu nchini Uchina ililosifiwa kwa kuvunja rekodi lilipozinduliwa siku 13 tu zilizopita limefungwa.
Maafisa wanasema serikali inapanga kufanya ukarabati wa dharura wa eneo hilo na hivyo kufunga daraja hilo Ijumaa, ambapo tarehe ya kufunguliwa tena itatangazwa.
Lakini Kituo cha televisheni cha Marekani CNN kimesema kuwa msemaji amewaambia kuwa daaja hilo linaloelea juu “limekuwa likitembelewa na wageni wengi kupita uwezo wake “.
Amesema kuwa hakuna ajali iliyowahi kutokea na daraja halikuwa na ufa wala mpasuko wowote.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 430, ambalo ujenzi wake uligarimu $3.4 milioni, linaunganisha mabonde mawili ya milima ya Zhangjiajie, katika jimbo la Hunan.
Daraja hilo Linaeloelea umbali wa mita 300 kutoka kwenye bonde linasemekana kuwavutia sana waandaaji wa filamu.
Lilipofunguliwa lilisemekana kuwa daraja refu zaidi kwa kimo na upana zaidi lililotengenezwa kwa vioo duniani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment