Ripoti ya Uwezo Tanzania Yaonyesha Hakuna Usawa wa Kielimu Licha ya Serikali Kutoa Elimu Bure

Pamoja na serikali ya awamu ya tano kuahidi kutoa elimu bure kwa ngazi ya elimu ya msingi na sekondari hadi kidato cha nne, imeelezwa kuwa bado kuna changamoto ya kukosekana kwa usawa kwenye vifaa vya shule na mazingira, uandikishaji na matokeo ya kujifunza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze wakati wa uzinduzi wa utafiti wa Uwezo Tanzania ya Je, Watoto Wetu Wanajifunza na kueleza kuwa kupitia tafiti hizo ni nafasi kwa serikali kuzitumia ili kuboresha elimu nchini kutokana na kukusanya takwimu katika sehemu nyingi ambazo zinaonyesha jinsi elimu ya Tanzania ilivyo kwa sasa.

“Mabadiliko mapya yanatekelezwa kwenye sera ya elimu na takwimu za Uwezo zinatoa fursa kwa watunga sera kufahamu ni wapi pa kuanzia … mamilioni ya watoto na vijana wetu wamepata nafasi ya kwenda shule kutokana na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi,

“Lakini takwimu hizi za Uwezo zinaonyesha kuwa wanafunzi wanahudhuria shule za msingi kwa miaka mingi bila kujifunza stadi za msingi za kusoma na kufanya hesabu. Ni lazima kujiuliza maswali maswali magumu nini ambacho tunavuna kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika shule zetu,” alisema Eyakuze.

Kwa upande wa Meneja wa Uwezo Tanzania, Zaida Mgalla alisema alisema katika tafiti hizo zilizofanywa kwa watoto wa darasa la tatu kusoma masomo ya darasa la pili, ilionekana watoto wengi wakifanya vizuri kusoma vitabu vya kiswahili lakini jambo hilo bado usawa unafanya kuwepo kwa tofauti kubwa kwa watoto wa familia maskini na zenye uwezo.

“Japokuwa inafurahisha kuona matokeo, hususani kwenye viwango vya ufaulu wa Kiswahili, matokeo bado hayajawa yanavyopaswa kuwa … kukosekana kwa usawa kwenye upatikanaji wa elimu, rasilimali, vifaa na ubora wa elimu kwa watoto wote inatisha sana,

“Watoto kutoka kaya zenye uwezo na maeneo ya mjini wana nafasi kubwa ya kuandikishwa katika shule za awali na shule za msingi. Pia wanao uwezo zaidi wa kupata vitabu na walimu shuleni, na hatimaye hufanya vizuri kuliko wenzao wa maeneo ya vijijini na wanaotoka kaya masikini. Mfumo wetu wa elimu unaonekana kuongeza matabaka ambayo wanapaswa kuyaondoa,” alisema Zaida.

Katika tafiti hizo zilizofanywa kwa watoto 32,694 wanaosoma darasa la tatu, 54% wanaweza kusoma hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili, 19% wanaweza kusoma hadithi ya Kiingereza ya darasa la pili na 35% wanaweza kufanya hesabu za darasa la pili.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment