Leo March 25 ripota wa millardayo.com aliongozana na mkuu huyo wa mkoa katika mitaa tofauti ikiwa ni pamoja na barabara ya Mwananyamala ili kujionea hatua zilizofikiwa na kukuta ukarabati ukiendelea…
Lakini bado mkuu wa mkoa hakuonyesha kuridhishwa na kazi iliyokuwa ikiendelea na kusema>> ‘Nilitoa siku 14 ukarabati wa hii barabara uwe umekamilika, nashukuru leo nimepita na nimekuta kazi imeanza, lakini nimewataka wahusika waangalie uwezekano wa kuwa na barabara za kudumu kwa muda mrefu‘ ;-Paul Makonda
‘Kuna barabara pale Makumbusho wamejenga alafu wameharibu mitaro, sasa nimemtaka mkandalasi arudi haraka na arekebishe, maana wamejaza mchanga kwenye mitaro, hatuwezi kuwa na barabara zisizokuwa na mitaro, baada ya siku kumi nitarudi tena kuhakikisha kama wamekamilisha‘ ;-Paul Makonda
Barabara ya kutokea Makumbusho kuelekea Mwananyamala
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda wakati akikagua barabara
Hiki ni kipande cha barabara ambacho bado hakijafanyiwa marekebisho
Wafanyakazi wakiendelea kupiga kazi
Hapa huruhusiwi kupita wakati ujenzi ukiendelea
Jamaa kataka kupenya wakamrudisha alipotoka
Watu wakipiga kazi
Jamaa akizibua moja ya mtaro ulioziba kwa uchafu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akicheki maendeleo
Barabara ya Mwananyamala sokoni
Barabara imefungwa ili kuzuia watu wasipite kuharibu utaratibu wa kazi
Mifereji pia imesafishwa kuondoa uchafu
Baada ya kuhakikisha kazi inaenda, mkuu wa mkoa na watu wake wakipiga stori
-via millardayo
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment