Ajali Mbaya ya Basi Yaua 6 Iringa Leo

ajali 
WATU 6 wamekufa na  wengine  38 kujeruhiwa  vibaya  baada  ya  basi lenye  namba  za  usajili    T 798 AKV mali ya Lupondije Express linalofanya safari za  Mwanza kwenda  Iringa  kupinduka  eneo la  Mteremko  wa Ipogolo  mjini  Iringa.
Mashuhuda wanasema kuwa basi hilo lililotakiwa kumalizia safari yake mjini Iringa lilipitiliza kwenda Ipogolo kwa minajiri ya kufaulisha abiria wachache wa Mbeya. Imeelezwa   kuwa baadhi ya  abiria    waliokufa  katika  ajali   hiyo na  majeruhi   ni  wale ambao   walitakiwa   kumaliza safari yao mkoani Iringa lakini dereva  wa basi  hilo aligoma   kuwashusha  na  kupitiliza kwenda Ipogolo    kufaulisha abiria  wa Mbeya  kwanza  ndipo arudi   kuwashusha  wa Iringa. 

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2 usiku jana baada ya basi hilo kufeli breki katika mteremko huo huo mkali kabla ya kupinduka katika eneo linalojulikana kama Kisima cha Bibi.
Wema Zuberi ni mmoja kati ya majeruhi wa ajali hiyo aliyekuwa ametoka mkoani Dodoma kuelekea Mbeya alieleza kuwa mwendo wa basi hilo haukuwa mkali bali kawaida.

Majeruhi huyo alieleza kuwa baada ya kuingia katikati ya mji wa Iringa ndipo dereva wa basi hilo alionesha kuendesha basi hilo kwa mwendo mkali zaidi kiasi cha baadhi ya abiria kulalamika mwendo huo na kutaka kushushwa ila dereva hakuwasikiliza zaidi ya abiria hao.

“Abiria wengi walionyesha kumlalamikia dereva huyo kwanza kutokana na kuwapitiliza stendi pasipo kuwashusha na pili mwendo kasi ambao alikuwa akienda nao ili kufanikisha kutufaulisha abiria tuliokuwa tukielekea Mbeya” alieleza
12920532_1094739447256715_3223310280829406857_n
Zaidi alisema, kabla ya kufika eneo hilo ambalo basi lilipinduka kuna kona kali na mteremko mkali na kilichoonekana haraka haraka ni dereva kushindwa kukata kona hiyo baada ya Breki kufeli na hivyo kulazimika kuhama njia na kugonga kingo za barabara hiyo na kupinduka .

Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema kuwa zoezi la kuendelea kutafuta miili iliyobanwa na basi hilo imekuwa ngumu kutokana na kukosekana kwa gari la kuinua basi hilo na tayari amemwagiza meneja wa Tanesco kuleta gari hilo na iwapo dereva hayupo basi

Hata hivyo alisema kuwa kuanzia sasa dawa ya madereva hao ni kuwashughulikia kwani kama Rai imekwisha tolewa mara nyingi na bado ajali zinaendelea kutokea.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa aliahidi kutoa taarifa mara tu zoezi hilo litakapokamilika kwa kuinua basi hilo na kutazama kwa kina kama kuna miili ambayo imefunikwa chini ama la.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia miili minne ikiwa tayari imetolewa katika basi hilo huku majeruhi wengi wakiwa wamepata majeraha makubwa mikononi ,miguuni na kichwani,Majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment