BARAZA LA MADIWANI LAMKATAA MKURUGENZI WA HALMASHAURI NA KUWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 4

Baraza la Madiwani Maalumu la Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara kwa pamoja limemkataa na kumkataza kushiriki shughuli zote za Halmashari hiyo Mkurugenzi Mtendaji Bw.Felix Mabula,kwa kutokuwa na imani naye na kuwasimamisha kazi watumishi wengine wanne kwa madai ya tuhuma za badilifu wa fedha zaidi ya shilingi Milioni 280,fedha ambazo zilikuwa za Halmashauri na uchaguzi.

Akitoa maamuzi hayo ambayo yameamuliwa kwa pamoja na Madiwani wote wa Chama cha CCM na vyama vya upinzani kutokana na taarifa ya Mkaguzi wa ndani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw.Geogry Bajuta amesema Baraza limetoa mapendekezo kwa Mamlaka husika kuwa Mkurugenzi huyo asimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi na amewataja waliosimamishwa kazi Mwekahazina Bw.Mazengo Matonya,Afisa Mipango Bw.Hamisi Katimba,Muhasibu Bi.Wellu Sambalu na Cashier Marseli Siima.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bw.Thobias Mwilapya amejikuta yupo katika wakati mgumu na kuamuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na Madiwani kukaa chini wakati alipokuwa amesimama akitoa salamu za Wilaya kwa madai ya kumpendelea mkurugunzi Bw.felix Mabula,hatimaye Mkuu wa Wilaya aliamua kutoka nje ya ukumbi.

Kwa upande wao Madiwani wa Hanang wameshangazwa na Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwa kuonyesha waziwazi kumkumbatia Mkurugenzi kwa madai ya kuwa kikao hicho siyo halali
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment