Kufuatia Mabadiliko ya Wajumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanywa na Mhe. Job Ndugai (Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana tarehe 22 Machi, 2016; baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii imenukuliwa ikihusisha mabadiliko hayo kuwa yamefanywa kutokana na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya Kamati za Bunge kufuatia ripoti ya chombo kimoja cha Habari.
Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, bali mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Spika ni ya kawaida na wala hayakuanisha dosari zozote katika Utendaji wa kamati za Kudumu za Bunge.
Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, bali mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Spika ni ya kawaida na wala hayakuanisha dosari zozote katika Utendaji wa kamati za Kudumu za Bunge.
Msingi wa Mabadiliko ya Wajumbe kwenye kamati, umelenga kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016 ambapo alikuwa ameanza kufanyia kazi mabadiliko hayo tangu mapema mwezi huu.
Waheshimiwa Wabunge wanaosakamwa kwa uvunjifu wa Maadili kupitia Mitandao ya kijamii na Magazeti, ni budi wakatendewa haki kwa sababu Mhe. Spika anazingatia sana Utawala wa Sheria na kama kuna Mbunge yoyote anaetuhumiwa kwa makosa ya Jinai, Mamlaka za kiuchunguzi zinawajibu wa kutekeleza majukumu yao na pale inapobidi, Bunge lenyewe kupitia kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inaweza kufanya uchunguzi kwa Mamlaka ya Spika.
Aidha, ifahamike vyema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) Mamlaka ya kufanya mabadiliko kwenye Kamati za Kudumu za Bunge ni ya Spika na anaweza kufanya hivyo wakati wowote kama alivyofanya mapema mwezi huu ambapo alizingatia maombi ya baadhi ya Wajumbe 15 kuhamia Kamati nyingine kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya kwa baadhi ya Wajumbe na pia kuboresha Utendaji wa Kamati hizo kama ilivyojitokeza jana kwa wajumbe 27 kuhamishiwa kamati zingine pia.
Mhe. Spika anawasihi Wajumbe wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida katika kamati zao.
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
23 Machi, 2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment