Mmoja wa Mashabiki wa Tamasha la
Pasaka pamoja na mashabiki wengine waliohudhuria katika Tamasha la
Pasaka lililofanyika mjini Geita Mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire
wakiimba kwa kuzunguka ukumbi huo wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa
akifanya vitu vyake jukwaani na kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo
kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti wakizunguka huku na kule huku
baadhi wakiwa wabebeba viti juu juu,
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
Mashabiki wake wakiitikia na kuimba kwa hisia wakati mwimbaji huyo akiimba jukwaani.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw.
Alex Msama akirekebisha sauti katika mitambo wakati tamasha hilo
likiendelea huku DJ akiangalia.
Mama akifurahia uimbaji na uponyaji kutoka kwa waimbaji katika tamasha hilo huku akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga.
Maadhi ya mashabiki wa muziki wa injili wakifuatilia waimbaji kwa makini.
Mwimbaji Martha Baraka na kundi lake wakitumbuiza jukwaani huku baadhi yamashabiki wakipata picha kwa simu.
Mwimbaji Jennifer Mgendi naye akafanya mambo makubwa jukwaani kama anavyoonekana.
Mwimbaji Ephraim Sekereti
akisalimiana na mdau mkubwa wa Msama Promotion Bw. Silas huku akitaniana
na Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie wa tatu kutoka kushoto
waliosimama mara baada ya kumaliza kuimba.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba jukwaani huku mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akicheza pamoja na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na mashabiki wengine.
Mwimbaji Solomon Mukubwa kutoka nchini Kenya akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake walioonekana kuhamasika na nyimbo zake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje naye akafanya mambo makubwa jukwaani huku akipewa sapoti na mashabiki wake.
Mwimbaji Bonny Mwaiteje akiwa
amewabeba wacheza shoo wake mara baada ya kumaliza kuimba jukwaani hii
ilikuwa ni staili ya aina yake.
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita
Manzie Mangachie akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama
Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya
Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie
Mungu na kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia ,
Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher
Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment