
Mgombea wa Republican nchini, Marekani Donald Trump.
Mgombea anayeongoza katika chama cha
Republican nchini Marekani Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama
mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na
Mississippi.
Wadadisi wanasema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi.

Wagombea wa Democratic Bernie Sanders na Hillary Clinton.
Baada ya kupata ushindi huo , Trump alisema kuwa anakiongezea
umaarufu chama cha Republican. Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye
alipata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.
Kwenye upande wa chama cha Democratic inaripotiwa kuwa Bernie Sanders
ameshinda mchujo katika jimbo la Michigan huku naye Hillary Clinton
akiibuka mshindi katika jimbo la Mississipi.
CHANZO: BBC SWAHILI
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment