Mahakama
kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo imetupilia mbali maombi ya James
Lembeli wa CHADEMA ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge wa
Jimbo la Kahama Mjini wa Oktoba 25 2015, kwa madai kwamba taratibu
zilikiukwa.
Akisoma
hukumu iliyochukua saa tatu Jaji wa Mahakama hiyo Moses Mzuna amesema
ushahidi uliotolewa na upande wa Lembeli haukuwa na nguvu za kutosha
kuishawishi mahakama hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi kwani sehemu
kubwa ni wa maneno.
Jaji
Mzuna amesema kitendo cha Lembeli kulalamikia vitendo vya rushwa
vidavyodaiwa kufanywa na mgombe wa kiti hicho kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Jumanne Kishimba kushindwa kuvitolea taarifa kwenye
vyombo vya dola kimedhoofisha ushahidi na kuuwekea mashaka.
Kwa
upande wa mashahidi waliounga mkono kuwepo kwa vitendo vya rushwa Jaji
Mzuna amesema wameshindwa kujenga hoja kwa mlolongo unaofanana kiasi
kwamba wameonekana kana kwamba walikuwa na ushahidi wa kutengenezwa.
Akitoa
hukumu hiyo, Jaji Mzuba amefafanua kuwa madai ya unyanyasaji wa wafuasi
wake waliokamatwa na polisi katika hoteli ya Golden Rock na wengine
katika kata ya Ngogwa yamekosa nguvu kufuatia kukosekana kwa kielelezo
cha maandishi kinachoonesha kwamba walikuwa mawakala wake.
Mzuna
amesisitiza, sababu ya Lembeli kushindwa kupeleka malalamiko kwenye
kamati ya maadili ya uchaguzi iliyowekwa kisheria kwamba hakuwa na muda
wa kutosha haikubaliki kwa kuwa mpiga kura yeyote anayemuunga mkono
angeweza kulalamika.
Kufuatia
uamuzi huo wa mahakama kutupilia mbali maombi ya kutengua matokeo hayo
Lembeli amesema anaiheshimu mahakama, na kwamba atashauriana na wakili
wake kuona kama haki haikutendeka ili kukata rufaa.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini aliyekuwa mlalamikiwa namba moja katika
shauri hilo Kishimba alipohojiwa amesema Jaji ametenda haki kama
walivyotenda haki wananchi wa Kahama kwa kumpa kura za ushindi katika
uchaguzi wa oktoba 25,2015.
Shauri
hilo lilikuwa limevuta hisia za wananchi wa Kahama na kuhudhuria kwa
wingi leo kwenye hukumu yake huku makundi ya kisiasa yaani wana-CCM na
wana-CHADEMA yakijionesha wazi kwa kushangilia bila dalili zozote za
uvunjifu wa amani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment