Kifo cha Kijana Huyu Chazua Utata Kijitonyama Jijini Dar [+PICHAZ]

AFIA NDANI (6)AFIA NDANI (1) Wakazi wa jirani wakielekea eneo la tukio. AFIA NDANI (12)Maiti ya Kijana Bocho ikichukuliwa na Jeshi la Polisi.
AFIA NDANI (3) AFIA NDANI (4)….Wkimiminika eneo la tukio. AFIA NDANI (5)    AFIA NDANI (9) AFIA NDANI (10) Wakazi wa Kwakopa, Kijitonyama wakitaharuki eneo la tukio.
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la utani la Bocho mkazi wa Kwakopa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, amefariki dunia huku kifo chake kikionekana kuwa na utata kutokana na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Mistlipenga kuendelea na shughuli zake bila ya hofu yoyote.

Tukio hilo la ajabu limegunduliwa na mmoja wa ndugu wa Mistlipenga mara baada ya kuingia ndani na kukuta Bocho akiwa amefariki huku mama yake akiendelea na shughuli zake za kila siku kama hajafiwa na ndipo alipoamua kwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Kopa.

“Tumeshangazwa na kitendo cha mama Bocho kuendelea na kazi bila kustuka kufariki kwa mwanaye, hii ni hatari, kifo cha huyu jamaa hakitakuwa cha kawaida, mama mtu akiulizwa anasema hajalala kwa jina la Yesu, duh!” alisema mmoja wa mashuhuda aliyekuwepo katika eneo la tukio.

Mwandishi wetu alishuhudia mama huyo akiendelea na shughuli zake kama kawaida na ndiyo chanzo cha utatata wa kifo cha kijana huyo ulipo, hata hivyo mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
Na Gabriel Ng’osha/GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment