Kutoka
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa
Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Lupa Mh. Victor Mwambalaswa.Wakijadiliana jambo
…Wakishuka kwenye gari mara baada ya kuwasili mahakamani hapo.…Wakielekea kwenye ofisi za mahakama. Wananchi waliofika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo. Wakijiandaa kutoka mahakamani.
Dar es Salaam
Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewaburuza kwenye Mahakama
ya Kisutu jijini Dar, wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotuhumiwa kuomba rushwa kiasi cha
Tsh. milioni 30 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mkoa
wa Morogoro.
Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la
Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na
Mbunge wa Mh.Victor Mwambalaswa. Hata hivyo Jaji Thomas Simba ambaye
amesikiliza kesi hiyo ameiahirisha hadi itakapotajwa tena Aprili 14,
2016, huku watuhumiwa wakiachiliwa kwa dhamana ya Tsh. milioni tano kwa
kila mmoja.
PICHA NA STORI: GABRIEL NG’OSHA/GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment