Siku kadhaa zilizopita bodi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) ilisitisha
msaada wa awamu ya pili wa kutoa zaidi Trilioni 1.4 kwa Tanzania
kutokana na kile lilichosema kuwa ni malalamiko ya uchaguzi wa Zanzibar
na sheria mpya ya makosa ya mitandao Tanzania ikisema Tanzania
iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao haukushirikisha wote na
haikujali malalamiko ya Marekani na jamii ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijini ‘REA‘ Lutengano Mwakahesya amezisikia taarifa kwamba moja ya miradi ambayo itakosa pesa hizo za msaada ni REA na sasa anatamka yafuatayo >>> ‘REA
haijawahi kupata fedha za MCC, REA imekuwa ikiendeshwa kwa fedha za
serikali ambapo imekuwa ikichangia kwenye mfuko huo kwa karibu 90% ya
fedha zote tunazofanyia kazi na hizo 10% ndio zinatoka kwa wahisani’
>>>’Shughuli
za REA haziwezi kusimama naserikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi
kwenye bajeti hii kwa hiyo kasi itakuwa kubwa zaidi’ – Mwakahesya.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment