Ujenzi wa daraja la Kigamboni ambalo linapita juu ya bahari ya hindi Dar es salaam kuwezesha wanaokwenda na kutoka Kigamboni kuvuka kwa urahisi bahari bila kutumia Pantoni, umekamilika kwa asilimia 90 na daraja litazinduliwa rasmi April 16 2016.
1. Kwenye
eneo la daraja hili kuna kituo cha Polisi chenye mpaka mahabusu hivyo
yeyote atakaezingua itakua rahisi kumshughulikia, pia kutakuwa na mizani
ya kupimia magari mazito pamoja na ofisi ya kulitazama au kufatilia
Daraja litakapoanza kutumika.
2.Watakaokuwa
wanapita watakuwa wanalipia kuvuka kupitia daraja hilo ndio maana kuna
ofisi au ‘vijiwe’ maalum ambavyo vitakua vinafanikisha process zote za
kulipia.
3.Pamoja
na kwamba bado daraja lenyewe halijaanza kutumika rasmi, Injinia
anaesimamia ujenzi huo ameomba Watanzania kujali na kuthamini kila
kilichopo kwenye daraja hilo na sio kuiba au kuharibu chochote, tayari
mpaka sasa Camera nne za video za kurekodi mienendo na usalama wa daraja
hilo zimeibiwa.
4.Ujenzi wa daraja hili ulianza
February mwaka 2012 na walitarajia wangemaliza ujenzi January 31 2015
lakini ikashindikana sababu Wajenzi walipata changamoto katikati ya
bahari, walichimba chini ya kitako cha bahari mita kama sitini na nne
lakini walipofika kwenye mita 56 wakagundua kulikua na pango chini,
wakaendelea kwenda chini mita 84.
5.Gharama za ujenzi kwa Mkandarasi ni shilingi za kitanzania BILIONI 214.6 ambazo kimkataba asilimia 25 zinalipwa kwa pesa za Kitanzania na asilimia 75 zinalipwa kwa dola za Kimarekani ambapo wakati wanafungua tenda Dola ya kimarekani ilikua shilingi 1590.
Kujua mengine zaidi bonyeza play kwenye hii video hapa chini…..
-millardayo
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment