Soo la Abdi Banda Lazua Makubwa SIMBA SC

Banda-2-1-682x1024 
Abdi Banda.
Khadija Mngwai, Dar es Salaam
BAADA ya kuibuka kwa sekeseke la wachezaji wa Simba, Abdi Banda na Hassan Isihaka kukwaruzana na kocha wao, Jackson Mayanja, kocha huyo amegusia suala la usaliti.
Mayanja amesema hayo baada ya kuanza kuenea kwa hisia kuwa mgogoro huo wa kocha na wachezaji unaweza kusababisha usaliti kwa wachezaji na kocha. Mayanja amesema kamwe hataogopa kusimamia nidhamu kisa akihofia kusalitiwa na wachezaji wake.

Mayanja ambaye ameshinda mechi 11 na kufungwa moja tu dhidi ya Yanga tangu alipoanza kuinoa Simba, amefunguka juu ya tetesi hizo kwa kusema:
“Mimi ndiye mkuu wa benchi la ufundi, hakuna mchezaji ambaye atapanda juu yangu, kila mchezaji anatakiwa kufuatisha kile ninachomuelekeza na sitasita kumuondoa yeyote kikosini kwa kuwa siwezi kukaa na kirusi ambacho kitawaharibu wachezaji wengine.

“Tatizo la wachezaji wa Kiafrika wamekuwa wakitaka kuwa juu ya mwalimu na kujiona wao mastaa na kuwajibu walimu bila ya sababu, mchezaji akitolewa anahoji kwa nini ametolewa uwanjani, akifanya kosa ukimrekebisha anatoa maneno yasiyofaa.

“Sitasita kuwaambia ukweli wachezaji wa Simba na sihofii kuhujumiwa maana kuna baadhi ya makocha wanahofia kuwaambia wachezaji ukweli kwa madai kuwa watawahujumu.
“Mmi ninafanya kazi yangu kama kocha kwa kufuata misingi ya profesheno yangu niliyosomea na sitamuonea mtu.
“Wajue kuwa jambo hili si kwa mchezaji mmoja tu, yeyote yule atakayefanya jambo kama hili sitasita kumuondoa kikosini.”
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment