Hamis Kiiza.
Khadija Mngwai, Dar es Salaam
MBIO za kuwania tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara
imeendelea kushika kasi hata nje ya uwanja ambapo kuna kampeni maalum ya
kuhakikisha tuzo hiyo inaenda kwa mchezaji fulani.
Mpaka sasa Hamis Kiiza wa Simba ndiye anayeongoza kwa kuwa na mabao
19, akifuatiwa na Amissi Tambwe wa Yanga ambaye ana mabao 17, lakini
wachezaji wa Yanga wamesema kuwa wanachotaka ni kufanya juu chini
mchezaji mwenzao ampiku Kiiza na kutwaa tuzo hiyo.
Tambwe.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amesema wamekubaliana kuongeza
nguvu uwanjani na kumtengenezea zaidi Tambwe ili afunge na kuiwezesha
timu yake kushinda na yeye kuwa mfungaji bora.“Mimi nilikuwa mfungaji
bora msimu uliopita, Tambwe amefikia idadi hiyo ambayo niliifikia msimu
huo, kwangu mimi hakuna tatizo katika hilo, kikubwa ni kuwa
tutahakikisha tunamsaidia Tambwe aweze kufanikiwa kuibuka mfungaji bora.
“Tumekubaliana wachezaji wote kuhakikisha tunampatia yeye pasi za
mwisho pale atakapokuwa vizuri ili kuweza kufanikiwa kufunga na kuongeza
idadi ya mabao yatakayomsaidia kusonga mbele.
“Tunafanya kazi kwa ushirikiano kwani lengo letu ni kuona
tunafanikiwa kutwaa ubingwa na kiatu hivyo kila mmoja yupo katika
kumsaidia Tambwe,” alisema Msuva.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment