Serikali ya Kenya imetangaza kuwafuta
kazi maafisa wakuu wa Baraza la Mitihani la nchi hiyo (KNEC) kutokana na
visa vya udanganyifu vilivyoripotiwa wakati wa mitihani ya kitaifa
mwaka jana.
Waliofutwa kazi ni pamoja na afisa mkuu
mtendaji wa baraza hilo Bw. Joseph Kivilu na mwenyekiti wa bodi
inayosimamia baraza hilo Bw. Kibiru Kinyanjui.
Bw Kivilu pamoja na maafisa wengine saba wa baraza hilo wametakiwa kuandikisha taarifa kwa polisi mara moja.
Tangazo la kufutwa kwa wakuu hao
limetolewa kwenye kikao cha wanahabari kilichoandaliwa na Waziri wa
Usalama na Masuala ya Ndani Meja Jenerali Joseph Nkaissery na Waziri wa
Elimu, Fred Matiang’i.
Waziri wa Elimu, Fred Matiang’i, Bw Matiang’i.
Watahiniwa waliopatikana na makosa ya
udanganyifu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2015 waliongezeka asilimia
70 kutoka mwaka uliotangulia. Katika mtihani wa mwaka 2015, watahiniwa
5,101 waligunduliwa kuwa walitumia udanganyifu katika mtihani.
Mwaka 2014, ni watahiniwa 2,975 pekee
waliokuwa wametumia hila katika mtihani huo wakati huo visa vikiwa
vimepungua kutoka visa 3,812 mwaka 2013.
Aliyekuwa naibu chansela wa chuo kikuu
cha Nairobi Prof George Magoha ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa bodi
hiyo na ataanza kufanya kazi mara moja.
Muda mfupi baada ya tangazo la kufutwa
kwa wakuu hao kutolewa, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa
wakieleza hisia zao na kitambulisha mada #KNEC kimeanza kuvuma.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment