HABARI NJEMA: Mradi Mwingine Ambao Utaleta Mapinduzi Makubwa ya Kiuchumi Nchini

Baada ya Tanzania kufanikiwa kuchukua mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda ambapo Bomba hilo linatarajiwa kujengwa kutoka Uganda mpaka Bandari ya Tanga na mradi huo ukikamilika utaliingizia Taifa bil 4.8 kila siku. 

Aprili 25 2016 Balozi wa China nchini Lu Youqing amekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo ambapo pia amemkabidhi barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa China Mheshimiwa Xi Jinping.
Balozi Lu amethibitisha China kuwa itashirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya kati yenye urefu wa kilometa 2,561 kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge” ambao zabuni za ujenzi zinatarajiwa kutangazwa hivi karibuni. 

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amemweleza Balozi Lu kuwa Tanzania imedhamiria kuanza ujenzi wa Reli ya kati haraka iwezekanavyo na tayari imetenga fedha kiasi cha shilingi Trilioni 1 katika bajeti yake ijayo kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi huo……..
>>>”Tuna imani kuwa mradi huu utasaidia kuleta mapinduzi makubwa ya uchumi katika nchi yetu na katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na kati zikiwemo Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndio maana hatutaki kupoteza muda kwa mazungumzo marefu, tunataka kazi ianze na watu waanze kunufaika“:- Rais Magufuli

Kwa upande wake Balozi China hapa nchini Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa kujiandaa kwa fedha, vifaa na rasilimali watu kwa ajili ya kutekeleza mradi huu mkubwa na kwamba Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni mbalimbali yatatoa ushirikiano wote katika utekelezaji wa mradi huu….. 
>>>”Kama ambavyo Prof. Mbarawa amefanya mazungumzo na Serikali ya China, Taasisi za fedha za China na Makampuni, naahidi kuwa tutaanza kazi kama ambavyo taratibu na viwango vya ujenzi vimewekwa, tutafanya kazi kwa kujali muda, ubora na gharama nafuu” :-Balozi Lu. 

Mradi mzima wa ujenzi wa reli ya kati unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 6.8 na umepangwa kutekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa kilometa 1,216 za kutoka Dar es salaam – Tabora – Isaka – Mwanza na itajengwa kwa ushirikiano wa Tanzania na China.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment