ZITTO KABWE Alivyochambua Utendaji wa Rais MAGUFULI Dhidi ya Mafisadi


April 25 2016 Chama cha ACT Wazalendo kimekutana katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake Kiongozi Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe amempongeza Rais Magufuli kwa kuanza katika eneo moja muhimu sana ambalo anasema ni msingi mkubwa wa kuanzishwa chama chao. 

Amelitaja eneo hilo kuwa ni la kupambana na ufisadi, licha ya kumuunga mkono kwa hatua hizo anazozichukua lakini amesema bado Rais hafanyi inavyopaswa na hapa ameainisha vitu ambayo Rais hajavigusa kabisa .. 

>>>’Kuna mambo ya muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipia Rais ameyakalia kimya mfano suala la tegeta Escrow, bado mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya bil 8 wazalishe au wasizalishe umeme, hivi ndio vikundi maslahi katika sekta ya nishati ambavyo bila kuvibomoa Rais ataonekana anachagua katika vita hii‘. 

>>>’Suala la hatifungani la zaidi trilioni 1.2 ambazo serikali yetu ilikopa kutoka benki ya Uingereza ni sawa kuwa kuna hatua tayari zimechukuliwa lakini Serikali imefikisha mahakamani ni wanaoitwa madalali wa rushwa hiyo, sio walioitoa wala walioipokea, hatifungani hii imeongeza deni la Taifa kwa kiwango cha trilioni 1.2 bila ya riba’. 

>>>’Tungetarajia Rais angewaongoza watanzania kukataa aina hii ya mikopo, lakini Takukuru wanaona ni sifa kuweka ndani watu wa dola mil 6 na kutusaulisha kabisa kwamba mkopo huu ambao kimsingi haupaswi kulipwa, ni wa trilioni 1.2 kwa hiyo katika vita dhidi ya rushwa sio swala la kutumbua majipu tu ni suala la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia kabisa rushwa katika nchi yetu na jambo hili bado serikali ya CCM hailifanyi’.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment