Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba, Haji Manara.
MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba, Haji Manara, amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya Bajaj. Manara amepata ajali hiyo usiku wa kuamkia leo wakati akiwa njiani kwenda kwa shangazi yake ambaye ni mgonjwa.
Taarifa za awali zilieleza Manara alichomoka kutokea ndani ya Bajaj wakati ilipogonga kitu, lakini baadaye yeye alielezea kwa kina alipozungumza na gazeti hili.
“Hakika nimeumia sana, nilikwenda hospitali na sasa niko nyumbani ninauguza majeraha mkononi na usoni.
“Kweli bado nina maumivu makali sana kwa kuwa ilikuwa hatari sana. Kama kungekuwa na gari nyuma yetu, basi ingenikanyaga na kusababisha madhara makubwa au hata kupoteza maisha,” alisema.
Manara alielezea zaidi: “Niliamua kuacha gari, nikachukua Bajaj kwa lengo la kuwahi kwa mgonjwa, shangazi yangu ni mgonjwa. Lakini tukiwa njiani, Bajaj ilipiga tuta na mimi nikachomoka na kuanguka barabarani na kuumia sana.”
Timu ya TanzaniaLeo inamuombea Manara nafuu apone haraka!
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment