WAKATI
Rais John Magufuli akisisitiza kuwa utumbuaji majipu utaendelea
kufanyika hadharani bila kificho, pigo jingine kwa waliotumbuliwa na
wanaosubiri kutumbuliwa, limetangazwa.
Akisoma
Mwelekeo wa Kazi za Serikali bungeni jana, Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, mbali na kusisitiza kuendelea kushughulikia watendaji wazembe,
wabadhirifu na wavivu, alitangaza kuwa Divisheni ya Mahakama ya Rushwa
na Ufisadi imeanzishwa katika Mahakama Kuu na itaanza kazi zake Julai
mwaka huu.
Hatua
hiyo ni pigo kwa watuhumiwa wa ufisadi ambao tangu Serikali ya Awamu ya
Tano ilipoingia madarakani, wamekuwa wakichukuliwa hatua hadharani ya
kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zao, kiasi cha
baadhi ya wanasiasa kushindwa kuvumilia na kujitokeza kulalamika.
Miongoni
mwa wanasiasa waliojitokeza kulalamikia hatua ya watuhumiwa hao
kuchukuliwa hatua ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Freeman Mbowe na aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho
katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Edward Lowassa.
Mahakama ya Rushwa
Mahakama
hiyo ni moja ya ahadi zilizonadiwa na Dk Magufuli katika Ilani ya
Uchaguzi ya CCM 2015-2020 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana,
akisema katika Hotuba ya Ufunguzi wa Bunge na kuirejea wakati wa
uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama na Siku ya Sheria Duniani.
Katika
maandalizi ya uundwaji wake, Jaji Kiongozi, Shaban Lila, aliwahi kusema
kwamba mahakama iliitisha wadau mbalimbali wa haki jinai, kuangalia
namna ya kuanzisha mahakama hiyo, ambapo mjadala ulikuwa ni kuanzisha
mahakama huru au kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu, kitakachopewa
kipaumbele cha kushughulikia mafisadi.
Akitangaza
kukamilika kwa mchakato huo jana, Waziri Mkuu Majaliwa alisema:
“Napenda kuliarifu Bunge kwamba Serikali imeanzisha Divisheni ya
Mahakama ya Rushwa na Ufisadi katika Mahakama Kuu itakayoanza kufanya
kazi Julai, 2016.”
Uharaka wa kesi
Mbali
na kuanza kufanya kazi kwa mahakama hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa pia
alisema kuwa Serikali itaimarisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP)
na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ili ziharakishe utoaji
wa haki.
Uimarishwaji
wa ofisi hizo pia unatokana na agizo la Rais Magufuli alilotoa siku
hiyo ya uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama na Siku ya Sheria Duniani,
alipotaka kesi za uhujumu uchumi na ufisadi ziendeshwe kwa kasi, ili
jitihada za Serikali za kupambana na matatizo hayo, zizae matunda.
Katika
hotuba hiyo ya Siku ya Sheria Duniani, Rais Magufuli alielezea
kushangazwa na kitendo cha ofisi ya DPP, kuchelewa kuwapeleka mahakamani
watuhumiwa waliokamatwa na ushahidi.
Alitoa
mfano wa watuhumiwa waliokamatwa na meno ya tembo, ambapo alitaja
Mahakama ya Kisutu kuwa ilikuwa na kesi 26 za watu walioshikwa wakiwa na
nyara za Serikali, lakini kesi hizo zikachukua zaidi ya miaka mitano
bila kufanyiwa uamuzi.
Dk
Magufuli alisema maelezo yaliyokuwa yakitolewa ni kwamba upelelezi bado
unaendelea wakati wahusika wa kufanya upelelezi huo wapo na washitakiwa
walishikwa wakiwa na vielelezo.
Alisema
inawezekana hakimu akawa anataka kutoa hukumu, lakini DPP na Polisi
wanaofanya uchunguzi, wanasema upelelezi unaendelea, jambo linaloonesha
tatizo lililopo la ucheleweshaji kesi.
Utumbuaji kuendelea
Katika
hotuba hiyo ya Majaliwa, iliyokwenda sambamba na makadirio ya bajeti ya
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17, alisema Serikali
itaendelea kuwawajibisha wale wote ambao hawataendana na Falsafa na
Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano, lakini akasisitiza kwamba
serikali itachukua hatua kwa kuzingatia na kufuata Sheria, Kanuni na
Taratibu za Utumishi wa Umma.
“Niwahakikishie
Watanzania kwamba hakuna mtumishi au mwananchi atakayeonewa au
kunyanyaswa katika hili. Hivyo wale wote ambao wako safi waendelee
kutimiza wajibu wao bila woga. Kazi zifanyike kwa weledi na kwa kasi
bila urasimu,” alisema.
Majaliwa
alisema katika kutekeleza falsafa ya Hapa Kazi Tu na ili Tanzania
ifikie uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 ni sharti kila mtu
afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu wa hali ya juu.
“Ili
yawepo mapinduzi ya kweli ya kuelekea kwenye uchumi wa Kati
tunaodhamiria ni lazima tuimarishe uwajibikaji na maadili kwa viongozi,
watendaji na kwa kila Mtanzania. Sote tumeshuhudia hatua zinazochukuliwa
na serikali dhidi ya watumishi wasio waadilifu, wanaotumia fedha za
umma na madaraka yao vibaya.
“Ndio maana tumeanza kwa nguvu kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma ili zielekezwe kwenye shughuli zenye manufaa kwa Watanzania walio wengi na si vinginevyo,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
“Ndio maana tumeanza kwa nguvu kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma ili zielekezwe kwenye shughuli zenye manufaa kwa Watanzania walio wengi na si vinginevyo,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Akizungumzia
utekelezaji wa Sera ya Utoaji Elimu Bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi
Kidato cha Nne, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ipo changamoto ya upungufu
mkubwa wa madawati baada ya kuanza kuandikisha watoto shule bila malipo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment