KAPOMBE Aitibulia Azam FC

Shomari Kapombe.
AZAM FC imesema kutokuwepo kwa beki Shomari Kapombe katika mchezo wao wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia kumevuruga mipango ya timu hiyo.
Kesho Jumapili saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, Azam itacheza mechi ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Esperance. 

Kapombe aliondoka nchini Alhamisi iliyopita kwenda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo kutokana na tatizo la kupumua alilolipata akiwa kambini Taifa Stars wakati ilipokwenda kucheza na Chad mechi ya kufuzu Kombe la Afrika 2017.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha Msaidizi wa Azam, Denis Kitambi, alisema ni pigo kubwa kumkosa Kapombe kwenye mchezo huo kwani amevuruga mpango wa kutumia mfumo wa 3-5-2.

Alisema Kapombe ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakitumika katika kuufanikisha mfumo huo kufanya kazi kwa ufanisi uwanjani.
“Pigo kubwa tulilonalo sasa ni kumkosa Kapombe katika mchezo huu, yupo Afrika Kusini kwa matibabu hali hii imevuruga mfumo wetu wa 3-5-2 hivyo tuna kazi ya kuweka sawa mambo.
“Mchezaji mwingine mwenye hatihati ya kutocheza ni Sure Boy (Salum Aboubakar) huyu anasumbuliwa na nyonga, itategemea na Jumapili ataamka vipi ndipo tujue kama atacheza au la,” alisema Kitambi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment