Kocha JULIO Bhana, Hiyo Haiwezekani Kabisa

jamhuri-kihwelo-julio_7x1b2xzte59i1v7gw0dl3m06b
Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
JUMATANO wiki hii beki wa Mwadui FC, Iddy Mobby alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mobby alionyeshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu kwa mara ya pili straika wa Yanga, Donald Ngoma ndipo mwamuzi Selemani Kinugani kutoka Morogoro akamtoa nje. 

Sasa kali zaidi ni kwamba, Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfutia beki wake huyo kadi hiyo nyekundu akidai alionyeshwa kimakosa.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Julio alisema kuwa Kinugani alimwonyesha Mobby kadi hiyo kimakosa kwa sababu yeye siyo aliyemchezea faulo Ngoma kwani aliyefanya hivyo ni kiungo wake Razack Khalfan.

“Kadi nyekundu aliyopewa Mobby ilikuwa ni ya uonevu kwani si yeye aliyemchezea faulo Ngoma bali aliyekuwa amefanya hiyo ni Razack, hivyo naiomba TFF imfutie adhabu hiyo mchezaji wangu,” alisema Julio.

Razack naye alipoulizwa alisema: “Kweli mwamuzi alimuonea Mobby kwani mimi ndiye niliyemchezea faulo Ngoma kwani alikuwa anakwenda kutufunga.”
Hata hivyo, picha za video za mchezo huo zinaonyesha wazi kuwa Mobby ndiye aliyemchezea rafu Ngoma hivyo kuzima madai hayo ya Julio na Razack.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment