Mkuu
wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwa mujibu wa utafiti
alioufanya, ombaomba walioko jijini Dar es Salaam baadhi yao
wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.
Akihojiwa
katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha redio, Makonda
alisema wapo watu ambao wanatumia mwanya huo kusambaza dawa za kulevya.
“Wapo
wanaotumia fursa hii kusambaza dawa za kulevya kwa sababu anavyopita
huwezi kumhisi kwa namna anavyoonekana, lakini watu hawa ni miongoni mwa
mawakala wa kusambaza dawa za kulevya,” alisema Makonda.
Makonda
aliwataka wakazi wa jiji hilo kushirikiana naye katika kuwaondoa
ombaomba hao ambao wengi wanatoka nje ya Da es Salaam na kwamba hakuna
tija kuendelea kuwaacha.
“Watanzania
tuna upendo sana lakini tunahitaji kutafakari kama kweli watu walioko
barabarani wakiomba kama kweli wanahitaji msaada huo au la,” alisema Makonda.
Alisema
kwa kuendelea kuwaacha ombaomba hao pia kutasababisha vijana ambao sasa
wanaomba barabarani kuwa watu hatari katika maisha yao ya baadaye kwani
wakikosa pesa wataingia katika shughuli za uporaji ili wapate fedha.
“Itafika
kipindi ataanza kuangalia kile alichokuwa anakikusanya wakati akiomba
na kile anachokipata akifanya kazi, ataona akifanya kazi hapati kiasi
kikubwa, ataamua kuwa mporaji,” alisema Makonda.
Makonda
alisema kwa mujibu wa utafiti alioufanya, asilimia 80 ya ombaomba
wanatoka nje ya Dar es Salaam na kesho operesheni ya kuwaondoa watu hao
itaanza rasmi huku wale ambao hawana ulemavu wowote wakikamatwa kwa
makosa ya uzururaji.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment