Watuhumiwa
hao ni Ali Juma (24) ambaye ni dereva wa gari namba T 113 DCV aina ya
Toyota Hiace iliyokuwa ikisafirisha watu hao na Joseph John (42), wote
wakazi wa Dar es Salaam. Mwingine ni Idi Juma (38), mkazi wa Iringa.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Leonard Paul alisema watuhumiwa wote
walikamatwa saa 8:00 usiku wa kuamkia Aprili 14 mwaka huu, katika eneo
la Misajini wakati gari hilo likiendelea na safari.
“Misajini
iko katika barabara kuu ya Hedaru - Mombo ambapo baada ya askari wetu
kupata taarifa za wasafiri hao, waliwafuatilia na kuwakamata,” alisema.
Alisema,
kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu
mkoani kwetu lakini chanzo chake pamoja na mambo mengine ni jiografia ya
mkoa yenye njia nyingi za panya.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment