Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametoa miezi
mitatu kwa vyama 21 ambavyo havijakaguliwa kuwasilisha hesabu zake.
Kauli
ya Jaji Mutungi imekuja siku nne baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad kutoa taarifa juu ya
ukaguzi wa hesabu katika vyama vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu,
CAG alieleza kati ya vyama hivyo, chama cha CUF pekee ndicho kilikuwa
kimepeleka hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita, kati ya Januari hadi
Juni 2015.
Alisema vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya
hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume na kifungu cha 14 cha Sheria ya vya
ma vya siasa namba 5 ya mwaka 1992.
Akizungumza jana nje ya
viwanja vya Bunge, Jaji Mutungi alisema ukaguzi wa fedha katika vyama ni
suala la kisheria na lina mchakato wake, akisisitiza kuwa ofisi yake
imeisoma taarifa ya CAG na inaifanyia kazi kwa kuvipa vyama hivyo miezi
mitatu.
“Kwa mujibu wa sheria tunatakiwa kuvikumbusha vyama kufanya ukaguzi na tulifanya hivyo mwanzoni mwa mwezi huu (Aprili).
"Tuliviandikia
barua vyama vyote. Ila kutokana na kuibuliwa kwa suala hili
tumeviandikia barua na kuvipa miezi mitatu kukamilisha hesabu zao,”
alisema.
Alisema ofisi yake haiwezi kuweka shinikizo kuhusu
suala hilo kwa maelezo kuwa jambo hilo linafanyika kwa matakwa ya
kisheria.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment