Watu walioathirika na mafuriko wakiwa hawana pa kuishi
Jackson Mpankuli, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara amesema kuwa, mafuriko hayo pamoja na mvua za masika yamesbabishwa na kuchepuka kwa Mto Lumemo uliongia kwenye makazi ya watu kufuatia mvua za masika zilizoanza mwishoni mwa Machi.
Mpankuli amewataja watoto waliofariki dunia kuwa ni Esther Kong’oa (12) mwanafunzi wa Darasa la VI katika Shule ya Msingi Ifakara na Rehema Lyakalyaka (12) mwanafunzi wa Darasa la IV katika Shule ya Msingi Mbasa.
Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema kuwa wanafunzi hao walifariki dunia wakijaribu kuogelea kwenye moja ya madimbwi yaliyotokana na mafuriko kwenye maeneo yao mara baada ya kutoka shule.
Amesema, mpaka sasa takribani watu 100 wamehifadhiwa kwenye kambi moja iliyotengwa kwenye Shule ya Msingi Lumemo baada ya nyumba zao kujaa maji na nyingine kuanguka.
“Mafuriko ya mwaka huu ni makubwa yanayoweza kuchukua muda mrefu hadi kwisha tofauti na mafuriko ya miaka ya nyuma yaliyokuwa yanatumia siku mbili hadi tatu tu” amesema.
Akizungumza akiwa katika kambi ya waathirika, mmoja wa waathirika hao Carolina Pindaki amesema, majira ya usiku wa saa 8 usiku alistuka baada ya kuona maji yakiingia ndani mwake ambapo aliamua kutoka nje na kukuta vifaa mbalimbali vya nyumbani na kuwa kuku wake walipelekwa na maji.
Mashaka Mbilinyi, Diwani wa Kata ya Viwanja Sitini amesema, mvua hiyo imesababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kata za Mbasa, Viwanja Sitini, lipangalala na Ifakara na kusababisha madhara katika Kata ya Lumemo, Mbasa na viwanja sitini.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment