Mmoja ya mwanamke aliyewahi kujeruhiwa na mume wake
Hayo yalibainishwa leo na Polisi wa Kituo cha Turiani WP 6103 PC Rehema wakati akichangia mada ya elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwenye warsha ya mradi mpya wa GEWE II unaofadhiliwa na Shirika la Msaada la nchini Denmark (DANIDA) wakishirikisha waandishi wa habari na wajumbe 22 wa kamati za vituo vya taarifa na maarifa vya vitongoji na vijiji.
PC Rehema amesema kuwa, kupitia elimu iliyotolewa na TAMWA chini ya mradi wa GEWE I, jamii ya vijiji vya tarafa hiyo imeweza kubadilika na kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kiasi kikubwa.
Amesema kuwa, kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo kwenye tarafa hiyo walikuwa wakipokea taarifa mbalimbali zikihusisha ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kwa wanawake, ubakaji na ulawiti watoto, mimba za utotoni na wanawake kutelekezwa huku wakiwa na familia na wanaume zao.
Awali Marcela Lungu, Ofisa Ustawi wa jamii kutoka TAMWA amesema, mradi wa GEWE I ulitekelezwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2012-14 kwenye wilaya 10 za Tanzania ikiwemo Mvomero – Morogoro, Luchingu- Newala, Ruangwa na mchinga- Lindi na Ilala na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lungu amesema kuwa, mradi mpya wa GEWE II unatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja 2016 kwenye Tarafa ya Turiani wilayani Mvomero, Ruangwa, Newala ma Kinondoni kufuatia kuonekana kwa uhitaji wa elimu hiyo kwenye maeneo hayo baada ya kuisha kwa mradi wa kwanza.
Willy Mtembelo, Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Mtibwa wilayani humo amesema kuwa, katika kukamilisha mradi wa GEWE I, walikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo wa jamii juu ya ukatili wa kijinsia.
Alizitaja changamoto zingine kuwa ni ushirikiano mdogo wa wanavijiji kunapotokea tatizo la ukatili wa kijinsia mfano ubakaji kwa mtoto.
Rispa Mgaya, Mwakilishi Mtendaji wa Kata ya Mtibwa amesema, mradi huo pia uliweza kuleta mafanikio mbalimbali ikiwemo jamii kupata uelewa wa sheria na haki baada ya kupata elimu kupitia warsha, mafunzo na mikutano ya wazi iliyowafahamisha sheria mbalimbali.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment